2 Kings 13:15-19

15Al-Yasa akasema, “Leta upinde na baadhi ya mishale,” naye mfalme akafanya hivyo. 16Al-Yasa akamwambia mfalme wa Israeli, “Shika upinde mikononi mwako.” Alipokwisha kuichukua, Al-Yasa akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme.

17 aAl-Yasa akasema, “Fungua dirisha la mashariki,” naye akalifungua. Al-Yasa akasema, “Piga mshale!” Naye akapiga mshale. Al-Yasa akasema, “Mshale wa ushindi wa Bwana, mshale wa ushindi juu ya Aramu! Utawaangamiza Waaramu kabisa huko Afeki.” 18Kisha akasema, “Chukua mishale,” naye mfalme akaichukua. Al-Yasa akamwambia, “Piga ardhi kwa hiyo mishale.” Akaipiga mara tatu, halafu akaacha.

19 bMtu wa Mungu akamkasirikia na akasema, “Ungepiga chini mara tano au sita, ndipo ungeishinda Aramu na kuiangamiza kabisa. Lakini sasa utaishinda mara tatu tu.”

Copyright information for SwhKC